Thursday 27 June 2013

Photos: Ufupi wa kaptura ya binti wa Obama wazua gumzo

Wakati baba yake, rais Barack Obama akiwa ziarani barani Afrika, binti mdogo wa rais huyo, Sasha, alikua jijini New York akifanya shopping huku amevaa kikaptura kifupi (short shorts, al maarufu kama daisy dukes.) Mapaparazzi walimpiga picha binti huyo akiwa mitaani na raha zake na kuuliza mitandaoni kama ni sahihi kwa binti wa miaka 12, kuvaa kaptura fupi hivyo. Kama kawaida za mitandaoni, kilichozuka ni ubishi mkali kati ya wanaoona si sahihi, hasa kwa binti ya rais, na wale wanaoona ni poa tu. Wewe upo kwenye camp ipi? Unaweza ruhusu binti yako avae kaptura kama hii?





No comments:

Post a Comment